SOMO: TAMBUA MAJIRA NA NYAKATI
Luka 19:41-46
41 Alipofika karibu aliuona mji, akaulilia,
42 akisema, Laiti ungalijua, hata wewe katika siku hii, yapasayo amani! Lakini sasa yamefichwa machoni pako.
43 Kwa kuwa siku zitakuja, adui zako watakapokujengea boma, likuzunguke; watakuzingira na kukuhusuru pande zote;
44 watakuangusha chini wewe na watoto wako ndani yako, wasikuachie jiwe juu ya jiwe, kwa sababu hukutambua majira ya kujiliwa kwako
45 Akaingia hekaluni, akaanza kuwatoa wale waliokuwa wakifanya biashara,
46 akiwaambia, Imeandikwa, Nyumba yangu itakuwa nyumba ya sala; lakini ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyang'anyi.
Katika mistari hiyo hapo tunaona safari ya Yesu kuelekea Yerusalemu na wakati akiwa njiani kabla ya kuufikia mji wa Yerusalemu aliuona. Lile neon “aliuona” lina mana kubwa sana kuliko unavyodhani.
Lile neno “aliuona” lina maana ya kwamba Yesu Kristo aliuangalia ule mji kwa jicho la ndani na kuona hali yake ya kiroho na ya kawaida ya sasa nay a baadae. Hali hiyo huwezi kuiona kwa macho haya ya nyama bali lazima uwe na macho ya ndani (rohoni). Yesu alipouangalia mji ule aliona hali halisi ya ule mji kwa wakati uliopo na pia laiona hali ya ule mji kwa wakati ujao.
Kilichomfanya Yesu aulilie ule mji si kwa sababu ya hali iliyopo (iliyokuwepo) bali ilikuwa ni kwa sababu ya hali ya mji kwa wakati ujao hali ambayo ilionyesha kwamba mji ule utavamiwa na kuzingirwa lakini cha kushangaza ni kwamba mji ule haukuchukua tahadhari zozote dhidi ya hali yake ya baadae ambayo ilikuwa mbaya sana………. Hiki ndicho kilichomfanya Yesu aulilie ule mji.
Hali iliyokuwepo kwa mji wa Yerusalemu ndiyo hali ambayo watu wengi wanayo au wanapitia siku za leo. Unaona katika biblia Mhubiri 3:1 Kila jambo lina majira yake. Ni kitu cha kushangaza sana kuona watu wanajisahau na kuishi kiholela utadhani kwamba kesho haipo kwa hiyo wanajikuta wakijisahau kwa habari ya maisha yao ya baadae. Lazima ujue ya kwamba kama leo ipo ina maana kua kesho inakuja. Kama wewe ni kijana leo ujue siku zinakuja utakuwa mzee. Hoja yanngu hapa sio habari ya siku zijazo bali hoja ninayotaka kuisisitiza hapa ni kwamba j unajua kuwa kuna wakati ujao? Je umejiandaaje kwa ajili ya wakati ujao?
Katika Mwanzo 8:23 inasema “muda nchi idumupo, majira ya kupanda, na mavuno, wakati wa baridi na wakati wa ari, wakati wa kaskazi na wakati wa kusi, mchana na usiku, havitakoma” Hayo maneno ukiyaona yamebeba maana ya muhimu ambayo ninatamani na uielewe. Kwamba maadamu dunia bado ipo basi nyakati na majira havitakoma. Kama kuna kupanda basi kuvuna kupo, kama kua baridi basin a joto lipo kama kuna mema basi na mabaya yapo. Hii inatufundisha kwamba usibweteke hata kidogo na hali ya maisha uliyonayo sasa maana kama hali ya maisha nzuri leo basi ujue kuna wakati wa mabaya unakuja; na kama una hali mbaya leo basi fahamu kabisa ya kuwa kuna wakat wa mema unakuja.
Si lengo langu kukutisha kwa habari ya siku zijazo lakini lengo langu ni kukusisitiza kuwa uchukue tahadhari ili mambo yatakapobadilika basi uwe umejiandaa kwa namna fulani
Kwa mujibu wa maneno ya Yesu katika Luka 19:41-46 utaona kuwa mjiule ulikuwa na nyakati mbili tofauti na kila nyakati zilikuwa na kitu ndani yake. Ebu tuzitazame hapa chini
1. WAKATI ULIOPO. Muda huu ulikuwa una mambo yafuatyo
• Muda wa amani (mafanikio)
• Muda uliobeba kujua au kutambua
• Macho yamefichwa yasione yajayo
2. WAKATI UJAO. Huu nao ulikuwa na mamb yafuatyo
• Adui kujengea boma
• Adui kuzingira na kuteka
• Kuangusha chini mtu/mji na watoto wake ndani yake
• Kumwondoa kabisa bila kuacha kumbukumbu yoyote
Huo hapo juu ndiyo mgawanyo wa nyakati katika mji wa Yerusalemu na ni halisi kwa maisha ya kila mmoja wetu. Kwa hiyo ninataka tujifunze juu ya nini cha kufanya katika wakati huu tulionao sasa. Haya mambo nitakayoyaeleza hapa yatakuwa ni mambo ambayo yanaweza kuwa msaada kwako wewe ambaye leo unaona uko katika hali njema ili uchukue tahadhari na kujiandaa kwa ajili ya wakati ujao. Na hata kama unaona kwamba unapita kwenye hali mbaya sana kimaisha bado haya mambo ninayoyaeleza hapa yanaweza kuwa msaada kwako kwa ajili ya kufungua ukurasa mpya kwenye maishha yako
MAMBO YA KUFANYA KATIKA WAKATI HUU WA SASA
1. Jenga boma kwa maombi. Ezekieli 22:30; Mathayo 26:41. Unapoona uko katika hali ya mafaniko huo ni wakati wako kujijengea boma kwa njia ya maombi. Katika destur za maeneo ya mashariki ya kati waliamini kuwa miji ili iwe salama ni lazima wajenge boma kuuzunguka mji; hii ilikuwa inasaidia kuongeza ulinzi wa mji dhidi ya maadui na watu wenye nia mbaya na mji huo. Nawe pia unapoona upo katika hali njema kimaisha au katika Nyanja yoyote ile hakikisha unajijengea boma la maombi. Sio lazima usubirie matatizo yaje ndipo uanze kuombana kumlilie Mungu. Unao wakati kwa kuomba leo ili Mungu akuepusha na mabaya ambayo shetani ameyaandaa kuja mbele yako. Yesu aliwambia wanafunze wake akasema “ombeni msije mkaingia majaribuni” Nami nakukumbusha leo hii ya kwamba usiache kuomba hata kama unaona kwamba huna shida hakikisha unjiombea maana hujui ni kitu gani shetani amekikusudia kwa ajili yako na kwa ajili ya maisha yako ya baadae. Tatizo ni kwamba watu wengi tunasubiri wakati wa matatizo ndipo tuanze kumwomba Mungu, hiyo ni tabia mbaya sana ndio maana utakuta wengi wetu wanastawi kiroho wakti wa kufanikiwa lakini ikitokea jambo la kuwayumbisha utaona wanakuwa imara kwa muda mfupi sana baadae wanapotea na hawawezi tena kuendelea kabisa na wokovu
2. Mkumbuke Bwana Mungu Wako (USIJIVUNE) Kumbukumbu 8:17. Kama unajiona kuwa umefanikiwa leo basi fahamu ya kwamba chanzo cha mafanikio yako ni Bwana. Kwahiyo hakuna haja ya kuanza kujivuna na kuona kwamba wewe ndiye uliyesababisha hayo mafaniko kwako bali unatakiwa uendelee kunyenyekea chini ya mkono wa Bwana. Watu wengi wamejikuta wakifa kiroho baada ya wao kufanikiwa maana wanasahau kwamba aliyefanikisha ni Mungu kwa hiyo wanapandisha mabega juu na kujiona wao ndiyo wao. Sikiliza nikuwambie leo kwamba kama unataka kundelea kuwa salama kwenye maisha yako hakikisha kuwa mafanikio uanyoyapata hayakufanyi ujivune. Unapojivuna unatengeneza hali ya Mungu kuondoa mkono na ulinzi wake kwenye maisha yako na matokeo yake ni mabaya sana kwako. Unapokuwa mnyenyekevu mbele za Bwana yeye Bwana ataendelea kuleta ulinzi wake juu ya maisha yako nawe utajikuta ukiendelea kustawi na kufanikiwa zaidi na zaidi….. Ayubu 1:8-10
3. Mtumikie Bwana Mungu – 1-Samwel 3:1; Daniel 6:20…. Kumtumikia Bwana ni kusimamia na kutekeleza kusudi la Bwana katika eneo ulilopo. Yawezekana ni kazini, shuleni, sokoni, kwenye biashara au kwenye eneo lolote ambalo upo unafanya shuguli zako za kila siku. Kumtumikia Bwana sio lazima kuwa muhubiri au mchungaji kama wengi wanavyodhani. Unaweza ukawa unamtumikia Mungu mahali pako pa kazi. Tunamwona Daniel katika biblia hakuwa muhubiri wala kuhani bali yeye alikuwa mtu aliyekulia kwenye jamii za kifalme kwa hiyo alikuwa ni mtu mwenye ujuzi wa mambo ya uongozi na utawala. Na hata alipopelekwa utumwani bado aliendelea na kazi za uongozi, utawala na usimamizi wa watu na shuguki mbalimbali Daniel 6:1.
Hii ina maana kwamba unaweza ukawa unamtumikia Mungu hapo kwenye shuguli zako za kipato cha kila siku huku ukiendelea na kazi yako. Kuna mawazo yaliyoenea kwa watu wengi kwamba kila anayetaka kumtumika Mungu lazima aache kazi au shuguli anayofanya; jambo hili sio kweli kabisa unaweza kumtumikia Mungu hata kama wewe uko kwenye ngazi ya juu serikalini; jambo la msingi na la kuzingatia ni kusimamia na kutekeleza jukumu la Mungu hapo kwenye mazingira ya kazi zako na shuguli zako. Unapomtumikia Mungu ina maana ya kwamba unatoa nafasi kwa Mungu kushugulika na maisha yako; na kama unasimamia kusudi la Mungu sawasawa utaona Mungu akikuepusha na mabaya ambayo shetani ameyapanga yakupate kama vile alivyoshugulika na Daniel alipotupwa kwenye shimo lenye samba wenye njaa hawakuweza kumdhuru. Ni kwa sababu alimtumikia Bwana. Ule utumishi alioufanya Daniel wakati akiwa kwenye nafasi ya utawala na uongozi ulimfanya Mungu amtetee na kumkinga na samba waliokuwa wanataka kumdhuru. Nawe pia ukisimamia kusudi la Mungu hapo ulipo Mungu atashugulika na maisha yako ya baadae na kukuondolea mabaya yote yaliyokusudiwa kuja kwako
Ninapomalizia somo hili leo nataka kukumbusha kuwa kila jambo lina majira yake lakini ni mbaya sana kwa mtu kukaa bila kuchukua tahadhari kwa habari ya mambo yajayo. Ni vema ukafuata hatua hizo tatu ambazo nimezieleza hapo juu ukazitekeleza; naamini hizo zitakuwa ni mtaji kwa ajili ya maisha yako ya baadae.
Mungu akubariki sana.
Uwe na wakati mwema
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
-
SOMO: TAMBUA MAJIRA NA NYAKATI Luka 19:41-46 41 Alipofika karibu aliuona mji, akaulilia, 42 akisema, Laiti ungalijua, hata wewe katika...
-
SHETANI ANAWEZA KUTUMIA KAZI YA MTU KUMLETEA MTU HUYO UHARIBIFU. Bwana YESU atukuzwe ndugu yangu. Karibu tujifunze Neno la MUNGU. L...
-
Katika Biblia, imeelezwa kuwa Sodoma na Gomora iliangamizwa na Mungu kwa sababu wakazi wa miji hiyo walizoelea maisha ya dhambi. Kwa mujib...
No comments:
Post a Comment