Wednesday, 5 December 2018

Kilichotokea Sodoma na Gomora

  Katika Biblia, imeelezwa kuwa Sodoma na Gomora iliangamizwa na Mungu kwa sababu wakazi wa miji hiyo walizoelea maisha ya dhambi. Kwa mujibu wa kitabu cha Mwanzo 19: 24-25, “Ndipo BWANA akanyesha juu ya Sodoma na juu ya Gomora kiberiti na moto toka mbinguni kwa BWANA. Akaangusha miji hiyo na Bonde lote, na wote waliokaa katika miji hiyo, na yote yaliyomea katika nchi ile.” Utafiti wa wanasayansi ambao matokeo yake yamewekwa wazi hivi karibuni, umethibitisha kile ambacho wasomi wa Biblia walikijua siku nyingi, kwamba maangamizi kutoka mbinguni yaliharibu mfumo wote wa maisha katika eneo la Bahari Mfu [Dead Sea] miaka maelfu kadhaa iliyopita. Baada ya kutumia karne nzima wakifanya uchunguzi, mwanaaikolojia Profesa Philip Salvian wa Chuo Kikuu cha Trinity Southwest kilichopo Albuquerque, New Mexico, Marekani, amezungumzia utafiti wake na wenzake, katika mkutano wa mwaka wa watafiti wa Kimarekani wa masuala ya Mashariki ya MbaliAmerican Schools of Oriental Research, hivi karibuni Wanasayansi hao wanaamini kuwa wamegundua maeneo ya miji hiyo kupitia uchunguzi wa kiaikolojia, lakini wametoa maelezo zaidi ya kisanyansi kwamba kwanini maeneo hayo yaliteketezwa kabisa. W a n a i k o l o j i a wanaeleza kuwa miji ile ilikuwa kaskazini mashariki ya Bahari Mfu [Dead Sea], ambako sasa panaitwa Middle Ghor. Kinachofurahisha ni kwamba katika maeneo hayo, wanasayansi wamegundua madini ya ajabu ambayo wanasema yanatokana na jiwe lililopasuka kutokana na joto kali katika ukanda huo. Mbinu za rediokaboni [ r a d i o c a r b o n ] zinaonyesha kuwa mlipuko huo wa jiwe ulitokea miaka kama 3,700 iliyopita-ambayo inaweza kuendana na muda wa kibiblia unaohusishwa na tukio hilo. Watafiti hao wameuita mlipuko huo wa jiwe kuwa ni 3.7KYrBP Kikkar na ulikuwa na kipimo cha megatani 10. [Megatani 1 ni sawa na kilotani 1000]. Muiakolojia huyo wa chuo kikuu cha Trinity Southwest ambaye pia ni mtafiti wa Biblia, Phillip Silvia anasema mlipuko huo unaweza kuathiri eneo lenye ukubwa wa kilometa 25, na kuangamiza makazi yoyote yaliyo karibu. Profesa Silvia anasema kuwa yeye na timu yake wamekuwa wakiufanyia utafiti mji wa Zama za Shaba wa Tall elHammam, karibu na Sodoma na Gomora, na ni eneo hilo ambalo linatoa ushahidi mkubwa wa mlipuko huo. Profesa Silvia na timu yake wameandika katika tovuti yao ya mradi wa utafiti katika eneo hilo-Tall el-Hammam Excavation Project: “Mji huo [unaweza kuwa] ulianza katika milenia ya 4 KK, na kustawi kwa miaka elfu moja kama eneo la wazi la jamii ya wakulima. “Lakini mwanzoni mwa milenia ya 3 KK, jambo la ghaf la kuhusiana na amani ya eneo hilo lililotokea, na kusababisha watu wa Tall el-Hammam kujenga mfumo wa kujilinda uliohusisha kujizungushia ukuta wa mawe na tofali za tope”. Silvia ameongoza utafiti katika maeneo makubwa matano ya Yordani pembezoni mwa Mto Yordani. Kwa mujibu wa Profesa Silvia, eneo lenye ukubwa wa maili za mraba 15 za Middle Ghor lilikuwa bonde lenye rutuba, likiendelea kukaliwa na watu kwa miaka kama 2,500 hivi. Maangamizi yaliyotokea miaka 3,700 iliyopita yalisababisha mwisho wa ghaf la wa mji huo, na kuteketeza watu wote wanaokadiriwa kuwa kati ya 40,000 hadi 65,000 walioishi katika eneo hilo wakati huo. Tukio hilo la maangamizi lilikuwa kubwa kiasi kwamba eneo hilo lilibaki bila kukaliwa na watu kwa miaka 600. Wasomaji wa Biblia wanafahamu kuwa miji ya Sodoma na Gomora iliteketezwa kwa moto baada ya Mungu kuihukumu kwa sababu ya uasherati uliokuwa ukifanyika ndani yake. Mwanzo 19:4-25. Katika kitabu cha Yuda 1:7 Biblia inasema: “Kama vile Sodoma na Gomora, na miji iliyokuwa kandokando, waliofuata uasherati kwa jinsi moja na hawa, wakaenda kufuata mambo ya mwili yasiyo ya asili, imewekwa kuwa dalili, wakiadhibiwa katika moto wa milele.”” Ikiwa Mungu aliwatenda hivi watu wa Sodoma na Gomora, ni kitu gani kinamfanya mwanadamu wa leo afikiri kuwa Mungu amebadilika juu ya kuadhibu wale wote wafanyao uasherati? Katika miji hiyo miwili ni watu watatu tu waliobaki ambao ni Lutu na watoto wake wawili. Wanadamu wengine wote waliokuwa katika miji hiyo waliteketezwa kwa sababu ya zinaa.

No comments:

Post a Comment