ROHO WA BWANA
GOD WITH US
Friday, 7 December 2018
ROHO MTAKATIFU ANAVYOONGOZA WANA WA MUNGU KUTEMBEA NA MUNGU KATIKA MAENEO MBALIMBALI YA MAISHA YAO (SEHEMU YA 1)
Jina la Yesu Kristo litukuzwe milele!
Leo nataka kuanza mfululizo mwingine wa somo, ambao naamini utakuwa wa msaada sana kwako, katika kuimarisha uhusiano wako na Mungu.
Somo lenyewe ni hili: “ROHO MTAKATIFU ANAVYOONGOZA WANA WA MUNGU KUTEMBEA NA MUNGU KATIKA MAENEO MBALIMBALI YA MAISHA YAO”.
Mfano na 1: Tunaposoma kitabu cha Matendo ya Mitume 27:10, tunaona jinsi mtume Paulo alivyoarifiwa na Roho Mtakatifu, juu ya hatari iliyokuwa mbele yake, katika safari aliyokuwa nayo na wenzake.
Mfano na 1: Tunaposoma kitabu cha Matendo ya Mitume 27:10, tunaona jinsi mtume Paulo alivyoarifiwa na Roho Mtakatifu, juu ya hatari iliyokuwa mbele yake, katika safari aliyokuwa nayo na wenzake.
Mtume Paulo akawaambia wenzake hivi: “naona kwamba safari hii itakuwa na madhara na hasara nyingi si ya shehena na marikebu tu, ila na ya maisha yetu pia”. Na jambo hili likatokea kweli kama alivyosema!
Swali la msingi la kujiuliza hapa ni kutaka kujua mtume Paulo alijuaje juu ya hatari ile! Roho Mtakatifu alitumia njia gani kumjulisha kwa uwazi namna ile? Je, na sisi leo Roho Mtakatifu anaweza kutujulisha juu ya hatari zilizo mbele yetu na tukauelewa ujumbe wake?
Mfano na 2: Je! Unafahamu mtume Paulo na wenzake walikuwa wanaamuaje juu ya eneo la kwenda kupeleka neno la Mungu? Ukisoma habari zao kwenye biblia, utajua ya kuwa ni kwa msaada wa uongozi wa Roho Mtakatifu.
Kuna wakati walikuwa wakipita nchi za Frigia na Galatia zilizokuwa Asia, wakitaka kulihubiri neno la Mungu huko. Biblia inasema walikatazwa “na Roho Mtakatifu, wasilihubiri lile neno katika Asia” (Matendo ya Mitume 16:6).
Biblia inaendelea kutueleza juu ya safari yao hiyo ya kwamba: “Walipofika kukabili Misia wakajaribu kwenda Bithinia, lakini Roho wa Yesu hakuwapa ruhusa” (Matendo ya Mitume 16:7). Na baada ya hapo, Roho akawapa kufahamu kuwa, walitakiwa kwenda Makedonia kuhubiri neno huko. Na ndivyo walivyofanya!
Swali la msingi la kujiuliza hapa, ni kutaka kujua walijuaje kuwa katika wazo walilokuwa nalo, Roho Mtakatifu alikuwa anawakataza wasilifanye, au anawanyima ruhusa wasilifanye? Na ikiwa Roho Mtakatifu ana wazo analotaka walitekeleze walilijuaje?
Je! Kwetu sisi – tulio wana wa Mungu kipindi hiki, tunaweza kupata msaada wa Roho Mtakatifu kuhusu mahali pa kwenda, au mahali pa kutokwenda, kama akina mtume Paulo walivyosaidiwa?
Na ikiwa ni hivyo – ina maana si suala la mtoto wa Mungu kuamua kwenda mahali popote atakavyo, bali hili ni muhimu ajue wazo la Roho Mtakatifu aliye naye ndani yake kuhusu safari yake hiyo!
Mfano na. 3: Roho Mtakatifu ndiye aliyemsaidia Yesu kuchagua wanafunzi wake kumi na wawili. Biblia inasema habari hizi za Yesu ya kuwa: “Ikawa siku zile aliondoka akaenda mlimani ili kuomba, akakesha usiku kucha katika kumwomba Mungu. Hata kulipokuwa mchana aliwaita wanafunzi wake; akachagua kumi na wawili miongoni mwao, ambao aliwaita Mitume” (Luka 6:12,13).
Habari hii haituambii moja kwa moja ni kwa namna gani, na kwa njia gani Yesu aliweza kufanya maamuzi ya nani amchague, na nani asimchague “miongoni” mwa wanafunzi wengi aliokuwa nao wakati ule!
Kwa msomaji yeyote wa biblia, anajua ni Roho Mtakatifu aliyemsaidia kufanya uchaguzi wa watu wa kukaa naye karibu! Lakini swali la kujiuliza ni kutaka kujua Roho Mtakatifu alimsaidia kwa njia zipi?
Nina uhakika tukijua jinsi Yesu alivyosaidiwa katika hili, itakuwa ni rahisi kwetu kusaidiwa na Roho Mtakatifu kujua watu wa kuwa nao karibu, na watu wa kukaa nao mbali! Pia naamini tunaweza kujua ni nani wa kushirikiana naye, na ni nani wa kutoshirikiana naye!
Biblia inasema katika Warumi 8:24 tunasoma ya kwamba: “wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu”.
Na Yesu akizungumza juu ya Roho Mtakatifu atakapokuja kwenye maisha ya wanafunzi wake alisema: “Lakini yeye atakapokuja huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote;…na mambo yajayo atawapasha habari yake” (Yohana 16:13).
Nataka ujue ya kuwa, ikiwa wewe ni mtoto au mwana wa Mungu, ni haki yako itokayo kwa Baba yako, yaani Mungu, kuongozwa na kutegemea kuongozwa na Roho Mtakatifu!
Uwe mtumishi wa Mungu au usiwe mtumishi wa Mungu – ili mradi tu wewe ni mtoto wa Mungu; Roho Mtakatifu uliye naye amepewa jukumu la kukusaidia, ikiwa ni pamoja na jukumu la kukuongoza katika maisha yako ya kila siku!
Ndani ya mfululizo wa somo hili, tutajifunza njia kadhaa anazotumia Roho Mtakatifu kumwongoza mwana wa Mungu.
Wednesday, 5 December 2018
Kilichotokea Sodoma na Gomora
Katika Biblia, imeelezwa
kuwa Sodoma na
Gomora iliangamizwa
na Mungu kwa sababu
wakazi wa miji hiyo
walizoelea maisha ya
dhambi. Kwa mujibu wa
kitabu cha Mwanzo 19:
24-25, “Ndipo BWANA
akanyesha juu ya Sodoma
na juu ya Gomora
kiberiti na moto toka
mbinguni kwa BWANA.
Akaangusha miji hiyo
na Bonde lote, na wote
waliokaa katika miji
hiyo, na yote yaliyomea
katika nchi ile.”
Utafiti wa wanasayansi
ambao matokeo yake
yamewekwa wazi hivi
karibuni, umethibitisha
kile ambacho wasomi
wa Biblia walikijua
siku nyingi, kwamba
maangamizi kutoka
mbinguni yaliharibu
mfumo wote wa maisha
katika eneo la Bahari
Mfu [Dead Sea] miaka
maelfu kadhaa iliyopita.
Baada ya kutumia
karne nzima
wakifanya uchunguzi,
mwanaaikolojia Profesa
Philip Salvian wa Chuo
Kikuu cha Trinity
Southwest kilichopo
Albuquerque, New
Mexico, Marekani,
amezungumzia utafiti
wake na wenzake,
katika mkutano wa
mwaka wa watafiti wa
Kimarekani wa masuala
ya Mashariki ya MbaliAmerican
Schools of
Oriental Research, hivi
karibuni
Wanasayansi hao
wanaamini kuwa
wamegundua maeneo
ya miji hiyo kupitia
uchunguzi wa
kiaikolojia, lakini
wametoa maelezo zaidi
ya kisanyansi kwamba
kwanini maeneo hayo
yaliteketezwa kabisa.
W a n a i k o l o j i a
wanaeleza kuwa miji
ile ilikuwa kaskazini
mashariki ya Bahari Mfu
[Dead Sea], ambako sasa
panaitwa Middle Ghor.
Kinachofurahisha ni
kwamba katika maeneo
hayo, wanasayansi
wamegundua madini ya
ajabu ambayo wanasema
yanatokana na jiwe
lililopasuka kutokana
na joto kali katika
ukanda huo.
Mbinu za rediokaboni
[ r a d i o c a r b o n ]
zinaonyesha kuwa
mlipuko huo wa jiwe
ulitokea miaka kama
3,700 iliyopita-ambayo
inaweza kuendana
na muda wa kibiblia
unaohusishwa na tukio
hilo.
Watafiti hao wameuita
mlipuko huo wa jiwe
kuwa ni 3.7KYrBP
Kikkar na ulikuwa na
kipimo cha megatani 10.
[Megatani 1 ni sawa na
kilotani 1000].
Muiakolojia huyo wa
chuo kikuu cha Trinity
Southwest ambaye pia
ni mtafiti wa Biblia,
Phillip Silvia anasema
mlipuko huo unaweza
kuathiri eneo lenye
ukubwa wa kilometa 25,
na kuangamiza makazi
yoyote yaliyo karibu.
Profesa Silvia anasema
kuwa yeye na timu yake
wamekuwa wakiufanyia
utafiti mji wa Zama
za Shaba wa Tall elHammam,
karibu na
Sodoma na Gomora,
na ni eneo hilo ambalo
linatoa ushahidi
mkubwa wa mlipuko
huo.
Profesa Silvia na timu
yake wameandika katika
tovuti yao ya mradi
wa utafiti katika eneo
hilo-Tall el-Hammam
Excavation Project: “Mji
huo [unaweza kuwa]
ulianza katika milenia
ya 4 KK, na kustawi kwa
miaka elfu moja kama
eneo la wazi la jamii ya
wakulima.
“Lakini mwanzoni
mwa milenia ya 3
KK, jambo la ghaf la
kuhusiana na amani ya
eneo hilo lililotokea,
na kusababisha watu
wa Tall el-Hammam
kujenga mfumo wa
kujilinda uliohusisha
kujizungushia ukuta wa
mawe na tofali za tope”.
Silvia ameongoza
utafiti katika maeneo
makubwa matano ya
Yordani pembezoni
mwa Mto Yordani. Kwa
mujibu wa Profesa Silvia,
eneo lenye ukubwa wa
maili za mraba 15 za
Middle Ghor lilikuwa
bonde lenye rutuba,
likiendelea kukaliwa na
watu kwa miaka kama
2,500 hivi. Maangamizi
yaliyotokea miaka 3,700
iliyopita yalisababisha
mwisho wa ghaf la wa mji
huo, na kuteketeza watu
wote wanaokadiriwa
kuwa kati ya 40,000
hadi 65,000 walioishi
katika eneo hilo wakati
huo.
Tukio hilo la
maangamizi lilikuwa
kubwa kiasi kwamba
eneo hilo lilibaki bila
kukaliwa na watu kwa
miaka 600.
Wasomaji wa Biblia
wanafahamu kuwa miji
ya Sodoma na Gomora
iliteketezwa kwa
moto baada ya Mungu
kuihukumu kwa sababu
ya uasherati uliokuwa
ukifanyika ndani yake.
Mwanzo 19:4-25.
Katika kitabu cha Yuda
1:7 Biblia inasema: “Kama
vile Sodoma na Gomora,
na miji iliyokuwa kandokando,
waliofuata
uasherati kwa jinsi moja
na hawa, wakaenda
kufuata mambo ya
mwili yasiyo ya asili,
imewekwa kuwa dalili,
wakiadhibiwa katika
moto wa milele.””
Ikiwa Mungu aliwatenda
hivi watu wa Sodoma
na Gomora, ni kitu gani
kinamfanya mwanadamu
wa leo afikiri kuwa
Mungu amebadilika juu
ya kuadhibu wale wote
wafanyao uasherati?
Katika miji hiyo miwili
ni watu watatu tu
waliobaki ambao ni Lutu
na watoto wake wawili.
Wanadamu wengine
wote waliokuwa katika
miji hiyo waliteketezwa
kwa sababu ya zinaa.
Tuesday, 13 November 2018
SOMO: TAMBUA MAJIRA NA NYAKATI
SOMO: TAMBUA MAJIRA NA NYAKATI
Luka 19:41-46
41 Alipofika karibu aliuona mji, akaulilia,
42 akisema, Laiti ungalijua, hata wewe katika siku hii, yapasayo amani! Lakini sasa yamefichwa machoni pako.
43 Kwa kuwa siku zitakuja, adui zako watakapokujengea boma, likuzunguke; watakuzingira na kukuhusuru pande zote;
44 watakuangusha chini wewe na watoto wako ndani yako, wasikuachie jiwe juu ya jiwe, kwa sababu hukutambua majira ya kujiliwa kwako
45 Akaingia hekaluni, akaanza kuwatoa wale waliokuwa wakifanya biashara,
46 akiwaambia, Imeandikwa, Nyumba yangu itakuwa nyumba ya sala; lakini ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyang'anyi.
Katika mistari hiyo hapo tunaona safari ya Yesu kuelekea Yerusalemu na wakati akiwa njiani kabla ya kuufikia mji wa Yerusalemu aliuona. Lile neon “aliuona” lina mana kubwa sana kuliko unavyodhani.
Lile neno “aliuona” lina maana ya kwamba Yesu Kristo aliuangalia ule mji kwa jicho la ndani na kuona hali yake ya kiroho na ya kawaida ya sasa nay a baadae. Hali hiyo huwezi kuiona kwa macho haya ya nyama bali lazima uwe na macho ya ndani (rohoni). Yesu alipouangalia mji ule aliona hali halisi ya ule mji kwa wakati uliopo na pia laiona hali ya ule mji kwa wakati ujao.
Kilichomfanya Yesu aulilie ule mji si kwa sababu ya hali iliyopo (iliyokuwepo) bali ilikuwa ni kwa sababu ya hali ya mji kwa wakati ujao hali ambayo ilionyesha kwamba mji ule utavamiwa na kuzingirwa lakini cha kushangaza ni kwamba mji ule haukuchukua tahadhari zozote dhidi ya hali yake ya baadae ambayo ilikuwa mbaya sana………. Hiki ndicho kilichomfanya Yesu aulilie ule mji.
Hali iliyokuwepo kwa mji wa Yerusalemu ndiyo hali ambayo watu wengi wanayo au wanapitia siku za leo. Unaona katika biblia Mhubiri 3:1 Kila jambo lina majira yake. Ni kitu cha kushangaza sana kuona watu wanajisahau na kuishi kiholela utadhani kwamba kesho haipo kwa hiyo wanajikuta wakijisahau kwa habari ya maisha yao ya baadae. Lazima ujue ya kwamba kama leo ipo ina maana kua kesho inakuja. Kama wewe ni kijana leo ujue siku zinakuja utakuwa mzee. Hoja yanngu hapa sio habari ya siku zijazo bali hoja ninayotaka kuisisitiza hapa ni kwamba j unajua kuwa kuna wakati ujao? Je umejiandaaje kwa ajili ya wakati ujao?
Katika Mwanzo 8:23 inasema “muda nchi idumupo, majira ya kupanda, na mavuno, wakati wa baridi na wakati wa ari, wakati wa kaskazi na wakati wa kusi, mchana na usiku, havitakoma” Hayo maneno ukiyaona yamebeba maana ya muhimu ambayo ninatamani na uielewe. Kwamba maadamu dunia bado ipo basi nyakati na majira havitakoma. Kama kuna kupanda basi kuvuna kupo, kama kua baridi basin a joto lipo kama kuna mema basi na mabaya yapo. Hii inatufundisha kwamba usibweteke hata kidogo na hali ya maisha uliyonayo sasa maana kama hali ya maisha nzuri leo basi ujue kuna wakati wa mabaya unakuja; na kama una hali mbaya leo basi fahamu kabisa ya kuwa kuna wakat wa mema unakuja.
Si lengo langu kukutisha kwa habari ya siku zijazo lakini lengo langu ni kukusisitiza kuwa uchukue tahadhari ili mambo yatakapobadilika basi uwe umejiandaa kwa namna fulani
Kwa mujibu wa maneno ya Yesu katika Luka 19:41-46 utaona kuwa mjiule ulikuwa na nyakati mbili tofauti na kila nyakati zilikuwa na kitu ndani yake. Ebu tuzitazame hapa chini
1. WAKATI ULIOPO. Muda huu ulikuwa una mambo yafuatyo
• Muda wa amani (mafanikio)
• Muda uliobeba kujua au kutambua
• Macho yamefichwa yasione yajayo
2. WAKATI UJAO. Huu nao ulikuwa na mamb yafuatyo
• Adui kujengea boma
• Adui kuzingira na kuteka
• Kuangusha chini mtu/mji na watoto wake ndani yake
• Kumwondoa kabisa bila kuacha kumbukumbu yoyote
Huo hapo juu ndiyo mgawanyo wa nyakati katika mji wa Yerusalemu na ni halisi kwa maisha ya kila mmoja wetu. Kwa hiyo ninataka tujifunze juu ya nini cha kufanya katika wakati huu tulionao sasa. Haya mambo nitakayoyaeleza hapa yatakuwa ni mambo ambayo yanaweza kuwa msaada kwako wewe ambaye leo unaona uko katika hali njema ili uchukue tahadhari na kujiandaa kwa ajili ya wakati ujao. Na hata kama unaona kwamba unapita kwenye hali mbaya sana kimaisha bado haya mambo ninayoyaeleza hapa yanaweza kuwa msaada kwako kwa ajili ya kufungua ukurasa mpya kwenye maishha yako
MAMBO YA KUFANYA KATIKA WAKATI HUU WA SASA
1. Jenga boma kwa maombi. Ezekieli 22:30; Mathayo 26:41. Unapoona uko katika hali ya mafaniko huo ni wakati wako kujijengea boma kwa njia ya maombi. Katika destur za maeneo ya mashariki ya kati waliamini kuwa miji ili iwe salama ni lazima wajenge boma kuuzunguka mji; hii ilikuwa inasaidia kuongeza ulinzi wa mji dhidi ya maadui na watu wenye nia mbaya na mji huo. Nawe pia unapoona upo katika hali njema kimaisha au katika Nyanja yoyote ile hakikisha unajijengea boma la maombi. Sio lazima usubirie matatizo yaje ndipo uanze kuombana kumlilie Mungu. Unao wakati kwa kuomba leo ili Mungu akuepusha na mabaya ambayo shetani ameyaandaa kuja mbele yako. Yesu aliwambia wanafunze wake akasema “ombeni msije mkaingia majaribuni” Nami nakukumbusha leo hii ya kwamba usiache kuomba hata kama unaona kwamba huna shida hakikisha unjiombea maana hujui ni kitu gani shetani amekikusudia kwa ajili yako na kwa ajili ya maisha yako ya baadae. Tatizo ni kwamba watu wengi tunasubiri wakati wa matatizo ndipo tuanze kumwomba Mungu, hiyo ni tabia mbaya sana ndio maana utakuta wengi wetu wanastawi kiroho wakti wa kufanikiwa lakini ikitokea jambo la kuwayumbisha utaona wanakuwa imara kwa muda mfupi sana baadae wanapotea na hawawezi tena kuendelea kabisa na wokovu
2. Mkumbuke Bwana Mungu Wako (USIJIVUNE) Kumbukumbu 8:17. Kama unajiona kuwa umefanikiwa leo basi fahamu ya kwamba chanzo cha mafanikio yako ni Bwana. Kwahiyo hakuna haja ya kuanza kujivuna na kuona kwamba wewe ndiye uliyesababisha hayo mafaniko kwako bali unatakiwa uendelee kunyenyekea chini ya mkono wa Bwana. Watu wengi wamejikuta wakifa kiroho baada ya wao kufanikiwa maana wanasahau kwamba aliyefanikisha ni Mungu kwa hiyo wanapandisha mabega juu na kujiona wao ndiyo wao. Sikiliza nikuwambie leo kwamba kama unataka kundelea kuwa salama kwenye maisha yako hakikisha kuwa mafanikio uanyoyapata hayakufanyi ujivune. Unapojivuna unatengeneza hali ya Mungu kuondoa mkono na ulinzi wake kwenye maisha yako na matokeo yake ni mabaya sana kwako. Unapokuwa mnyenyekevu mbele za Bwana yeye Bwana ataendelea kuleta ulinzi wake juu ya maisha yako nawe utajikuta ukiendelea kustawi na kufanikiwa zaidi na zaidi….. Ayubu 1:8-10
3. Mtumikie Bwana Mungu – 1-Samwel 3:1; Daniel 6:20…. Kumtumikia Bwana ni kusimamia na kutekeleza kusudi la Bwana katika eneo ulilopo. Yawezekana ni kazini, shuleni, sokoni, kwenye biashara au kwenye eneo lolote ambalo upo unafanya shuguli zako za kila siku. Kumtumikia Bwana sio lazima kuwa muhubiri au mchungaji kama wengi wanavyodhani. Unaweza ukawa unamtumikia Mungu mahali pako pa kazi. Tunamwona Daniel katika biblia hakuwa muhubiri wala kuhani bali yeye alikuwa mtu aliyekulia kwenye jamii za kifalme kwa hiyo alikuwa ni mtu mwenye ujuzi wa mambo ya uongozi na utawala. Na hata alipopelekwa utumwani bado aliendelea na kazi za uongozi, utawala na usimamizi wa watu na shuguki mbalimbali Daniel 6:1.
Hii ina maana kwamba unaweza ukawa unamtumikia Mungu hapo kwenye shuguli zako za kipato cha kila siku huku ukiendelea na kazi yako. Kuna mawazo yaliyoenea kwa watu wengi kwamba kila anayetaka kumtumika Mungu lazima aache kazi au shuguli anayofanya; jambo hili sio kweli kabisa unaweza kumtumikia Mungu hata kama wewe uko kwenye ngazi ya juu serikalini; jambo la msingi na la kuzingatia ni kusimamia na kutekeleza jukumu la Mungu hapo kwenye mazingira ya kazi zako na shuguli zako. Unapomtumikia Mungu ina maana ya kwamba unatoa nafasi kwa Mungu kushugulika na maisha yako; na kama unasimamia kusudi la Mungu sawasawa utaona Mungu akikuepusha na mabaya ambayo shetani ameyapanga yakupate kama vile alivyoshugulika na Daniel alipotupwa kwenye shimo lenye samba wenye njaa hawakuweza kumdhuru. Ni kwa sababu alimtumikia Bwana. Ule utumishi alioufanya Daniel wakati akiwa kwenye nafasi ya utawala na uongozi ulimfanya Mungu amtetee na kumkinga na samba waliokuwa wanataka kumdhuru. Nawe pia ukisimamia kusudi la Mungu hapo ulipo Mungu atashugulika na maisha yako ya baadae na kukuondolea mabaya yote yaliyokusudiwa kuja kwako
Ninapomalizia somo hili leo nataka kukumbusha kuwa kila jambo lina majira yake lakini ni mbaya sana kwa mtu kukaa bila kuchukua tahadhari kwa habari ya mambo yajayo. Ni vema ukafuata hatua hizo tatu ambazo nimezieleza hapo juu ukazitekeleza; naamini hizo zitakuwa ni mtaji kwa ajili ya maisha yako ya baadae.
Mungu akubariki sana.
Uwe na wakati mwema

Friday, 9 November 2018
NJIA ZA KIBIBLIA ZA KUKUSAIDIA KUMJUA MWEZI WAKO WA MAISHA
NJIA ZA KIBIBLIA ZA KUKUSAIDIA KUMJUA MWEZI WAKO WA MAISHA.
*Kwa kumcha MUNGU, ( kumtii MUNGU ).
*Kwa sauti ya MUNGU mwenyewe.
*Amani ya KRISTO.
*Upendo wa ki –MUNGU ( wa Dhati ).
*Mafunuo ya ki-MUNGU.
*Kwa kuyatenda mapenzi ya MUNGU.
*Kulijua kusudi la MUNGU katika maisha yako.
*Kuomba sawasawa na mapenzi ya MUNGU.
*Wazazi /walezi/wachungaji/kiongozi wako katika kundi lenu.
*Dhamiri za watu wengine au ushuhuda wa watu wengine.
BWANA MUNGU akubariki na akutangulie katika safari hii ya maamuzi makubwa katika maisha yako.
Wednesday, 7 November 2018
MAMBO YA KUFANYA/KUZINGATIA KATIKA KIPINDI CHA UCHUMBA
Baada ya kuwa tumepata maombi ya vijana wengi kutaka kujifunza habari za Uchumba, mke wangu pamoja nami tumeona ni vema tukaandaa somo hili ambalo tunaamini litafanyika msaada kwa vijana wengi ambao wapo kwenye uchumba au wanajiaandaa kuingia katika eneo hili. Hata hivyo somo hili ni pana sana, kwa sasa tumeandika vitu vichache vya msingi, tunaamini kwamba huko mbele tutaandika kitabu chake rasmi.
Katika kitabu cha Muhubiri 3:1 Biblia inasema “Kwa kila jambo kuna majira yake, na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu”. Hivyo mwanadamu katika maisha yake hapa chini ya jua kuna vipindi mbalimbali anavyovipitia hii ni pamoja na kipindi cha uchumba kwa sehemu kubwa ya watu.
Katika kipindi hiki yapo mambo mengi ambayo wachumba hufanya, mengine ni mazuri na mengine hayafai kabisa. Na hii yote inatokana hasa na mitazamo au tafsiri ya uchumba kwa watu husika. Fahamu kwamba tafsiri unayokuwa nayo juu ya mchumba wako ndiyo inayokuongoza kujenga mahusiano ya aina fulani pamoja naye.
Lengo la somo hili ni;
Kuongeza ufahamu wa wachumba kuhusu kipindi hiki na Kuwapa vijana maarifa ya kuwasaidia kuishi kwa nidhamu ya Ki-Mungu katika uchumba wao. Pia ni kuwafikirisha vijana wanaotarajia kupita katika kipindi hiki mambo ya kuzingatia. Si wachumba wengi wanajua, Mungu anawataka wafanye nini katika uchumba wao au kwa lugha nyingine si wachumba wote wanaojua kwa nini kipindi cha uchumba kipo. Naam katika somo hili tumeandika mambo hayo kinaga ubaga.
Kwa kuwa suala la uchumba ni pana na lina mitazamo mingi, yafuatayo ni mambo tuliyozingatia katika uandishi wa somo hili;
- Kuna makundi mbalimbali ambayo yana taratibu zao kuhusu mchakato wa mtu kumpata mke au mume kikiwepo kipindi cha uchumba. Makundi hayo ni pamoja na makanisa, makabila, familia nk.
- Wachumba wanaweza kutofautiana kwa kiwango cha elimu, uchumi, ufahamu juu ya mambo mbalimbali, kikabila, umri na hata kwa rangi pia.
- Kuna baadhi ya wachumba hadi kufikia muda wanakubaliana kwamba watakuja kuishi pamoja walishafahamiana tangu zamani na wengine hawakufahamiana.
- Wachumba wanaweza wakatoka katika madhehebu/makanisa tofauti na hili ni kwa kuzingatia madhehebu/makanisa mengi yaliyopo.
Lengo letu ni kuandika juu ya mwongozo wa Neno la Mungu katika kipindi cha uchumba. kwa lugha nyingine, je Mungu anataka wachumba wafanye nini katika kipindi chao cha uchumba?. Kumbuka uchumba ni kipindi/wakati. Basi kama ni wakati jua kabisa kuna baadhi ya mambo ambayo ni lazima yafanyike, kwani Biblia inasema katika Mhubiri 8:5b “ Na moyo wa mwenye hekima hujua wakati na hukumu”, neno hukumu linamaanisha maamuzi, mambo ya kufanya.
Yafuatayo ni mambo ya msingi kufanya katika kipindi cha uchumba;
Jambo la kwanza – Mruhusu Roho Mtakatifu afanyike Bwana wa uchumba wenu
2Wakorinto 3:17 ‘Basi Bwana’ ndiye Roho; na alipo Roho wa Bwana, hapo ndipo penye uhuru’.
Kumbuka Roho Mtakatifu ni msaidizi. Hivyo basi ni vema kumtumia vema hasa katika nyanja hii ya mahusiano katika kipindi hiki cha uchumba. Ni Roho Mtakatifu pekee mwenye uwezo wa kukujulisha mambo na siri nyingi kuhusu mchumba wako hata kama yeye hataki kukueleza. Ukimruhusu Roho Mtakatifu afanyike Bwana, yeye atakuongoza katIka kufanya maombi yanayolenga maeneo ya msingi juu ya huyo mwenzako. Kila mtu ameumbwa pamoja na mapungufu fulani au kwa lugha nyingine mapungufu/ udhaifu (weakness) ni sehemu ya maisha ya mwanadamu. Roho Mtakatifu anapokuwa Bwana wa mahusiano yako yeye atakusaidia kuona madhaifu au mapungufu ya mwenzako kama kitu cha wewe kujivunia(Strength) kwa maana ya kuona udhaifu wa mwenzako kama kitu chema na si kibaya.
Kumbuka Paulo katika 2Wakorinto 12:9-10. —‘Basi nitajisifia udhaifu wangu kwa furaha nyingi, ….kwa hiyo napendezwa na udhaifu——- maana niwapo dhaifu ndipo nilipo na nguvu. Hivyo Roho Mtakatifu atabadilisha tafsiri ndani yako za vyote unavyoona kwa mwenzako huenda juu ya umbile lake, umri wake, macho yake, kabila lake viwe vitu vya wewe kujivunia. Zaidi Roho Mtakatifu pia atakuongoza katika maombi yatakayosidia kuuondoa ule udhaifu ambao umekuja si katika mapenzi ya Mungu, yaani wa kishetani.
Jambo la pili – ni wakati wa kuweka msingi imara wa uchumba wenu na kufahamiana zaidi.
Hili jambo ni la muhimu kuzingatia. Ni vema wachumba wakatafsiri na kuelewa vizuri maana ya uchumba. Wachumba wanapaswa kuwa na mipaka fulani katika uchumba wao na kuwa makini kwa kujilinda na mazingira ya kila namna ambayo yanaweza yakapelekea wao kuanguka dhambini. Ni vema mkajua kwamba ninyi ni wachumba na si wanandoa. Na kama ni wachumba basi uchumba una mipaka yake na hamruhusiwi kufanya mambo ya wanandoa. Mipaka hii iwe kwa habari ya kutembeleana,kupeana zawadi, mawasiliano (ingawa mnapaswa kuwa makini na lugha mnazotumia pia) nk. Lengo la kutafsiri misingi ya mahusiano yenu ni kujiwekea mipaka na mazingira yatakayowasaidia kuishi maisha ya nidhamu, ushuhuda na kumletea Mungu utukufu.
Sambamba na hili sehemu kubwa ya wachumba huwa wanakuwa hawafamiani vizuri. Japo wapo baadhi ambao walianza tangu shule za msingi/sekondari/chuo na sasa wamechumbiana hivyo kwa sehemu wanafahamiana vema. Kwa wale wasiofahamiana vema huu ni wakati wa kumjua mwenzako vizuri kwa maana ya kabila lake, familia yake, umri wake, interest zake, matatizo aliyo nayo yeye binafsi au ya kifamilia, mitazamo yake juu ya mambo mbalimbali kama uchumba, ndoa, maisha, wokovu, neno la Mungu nk. Huu ni wakati wa kumjua mwenzako kwa njia ya maswali mbalimbali ya msingi yanayohusu vitu nilivyovitaja hapo juu. Lengo hapa ni kujua mapungufu/madhaifu(weakness) na mazuri(Strength) za mwenzako ili mjue namna ya kukabilana na mapungufu na namna ya kuendeleza yaliyo mazuri.
Ni vema pia kuulizana historia zenu za maisha ya nyuma. Kabla ya kuokoka umepitia katika mifumo gani ya maisha ambayo imechangia kukufanya uwe ulivyo. Kabla ya kumpata uliye mpata ulikuwa umefuatwa na wangapi na uliwakubalia au la, na kama uliwakubali kwa nini mliachana, na sasa wako wapi, je bado wanakufuatilia. Hii itawasaidia sana kujipanga vizuri kimaombi na katika mahusiano yenu na zaidi itawasaidia kuweza kuchukuliana na kuhifadhiana katika madhaifu ya kila mmoja.
Mungu anapowaunganisha anakuwa na kusudi maalum. Hivyo jua kwamba huyo mwenzi uliyepewa umepewa kwa ajili ya kusudi fulani la Mungu. Ni wachumba wachache sana ambao pindi wanapokutana kila mmoja anakuwa anajua walau kwa sehemu kwa nini aliumbwa. Sasa ni vema mkae chini mfikiri, nini Mungu anataka kukifanya duniani kupitia ninyi? Na zaidi angalieni kazi zenu au yale mnayoyasomea, Je mtawezaje kuliimarisha agano la Bwana kwa pamoja kama mke na mume?.
Hapa maana yetu mnatakiwa kujibu maswali yafuatayo? Je ni kwa nini mlizaliwa? Je kwa nini Mungu amekuunganisha na huyo uliye naye sasa? Na je kupitia elimu, bisahara zenu au kazi mlizonazo mtawezaje kuimarisha agano la Bwana?, Kwa kuzingatia vipawa na uwezo Mungu aliowapa, je ni wapi Mungu anataka kuwapeleka na kuwafikisha? Kama ndani yenu mna huduma fulani, je ni watu gani ambao Mungu atataka mshirikiane nao katika huduma hiyo?, je ipi ni nafasi yenu katika mwili wa Kristo na taifa kwa ujumla? Ni vema zaidi mwanaume akajua wito/ kusudi aliloitiwa ili pia amshirikishe na mwenzake.
Kufanikiwa kwa hili kunahitaji uwepo muda wa kutosha wa wachumba kukutana ili kupanga na kuweka mambo yao mbalimbali, na kama ni watu walioko mbali basi suala la mawasiliano kwa njia mbalimbali kama simu, barua pepe, na barua na hata zawadi ni la muhimu.
Jambo la tatu– ni wakati wa kulinda wazo la Mungu hadi litimie.
Siku zote uamuzi wowote unaoufanya una gharama. Naam uchumba pia una gharama nyingi Sana za kuzikabili kuliko unavyofikiri. Gharama hizo ni pamoja na muda, pesa, mawasiliano, maombi, uhuru nk. Kumpata mchumba au mwenzi ambaye ni wa kusudi la Mungu, usidhanie ndio umemaliza. Kama huo uchumba wenu ni wa mapenzi ya Mungu muwe na hakika mtakutana na vita kubwa sana katika kipindi hicho cha uchumba na lengo ni kuwatenganisha. Ni lazima mjifunze siku zote kuombeana kwa kumaanisha maana Shetani naye yupo kazini ili kuvuruga hayo mahusiano.
Kumbuka huyo mwenzi ni agano toka kwa Bwana hivyo unawajibika kumlinda, kumlinda ni pamoja na kuhakikisha wewe hausabibishi au haufanyiki chanzo cha ninyi wawili kuanguka dhambini, au ukamwacha na kumsababishia majeraha ya nafsini na hivyo kuharibu mahusiano yake na Mungu. Wapo watu waliofikia kuharibu mahusiano yao na Mungu kisa mchumba, saa ya ibada imefika mchumba anasema twende zetu out bwana, unataka kufanya maombi ya kufunga mchumba anasema kesho nitakutoa out, inagharimu sana muda wa kuwaza pia kwa ajili yake na familia yake au mahitaji mbalimbali aliyo nayo.
Zaidi pia uchumba unaweza kukunyima uhuru hata wa kuwa na maongezi na rafiki zako, maana kuna baadhi ya watu huwa hawataki kuona mchumba wake anaongea au kucheka na watu wengine, na pia kuna wengine ni wachumba lakini wamewekeana taratibu ngumu utafikiri wanandoa kabisa na ukweli zinawatesa ila kwa sababu hataki kumpoteza huyo mchumba wake inabidi avumilie. Jambo tunalosisitiza hapa ni kwamba, uchumba una gharama nyingi angalia mahusiano yako na Mungu yasiharibikie hapa.
Jambo la nne– ni wakati wa kupanga malengo na mikakati yenu ya baadae.
Mithali 29:18a “Pasipo maono, watu huacha kujizuia’
Hili si jambo ambalo vijana wengi hulipa kipaumbele linavyostahili. Katika hili ni vema wachumba wafikirie mapema ni aina gani ya maisha ambayo wangependa kuwa nayo, na pia je ni aina gani ya ndoa wanataka kufunga, tatu je ni wapi wangependa kuja kuishi kwa maishayaoyote. Haya yatawasaidia wahusika kujipanga ndani na nje kukabiliana na yaliyo mbeleyao.Kamawanataka kufunga harusi kanisani basi maana yake wanahitaji kuwa na maandalizi mazuri kifedha, waweke katika muda kila wanalotaka kuelekea katika harusiyaoili iwasaidie kujiaadaa mapema. Malengo yoyote yale ambayo mtaweka basi hakikisheni yanatekelezeka, yanafikika, yanapimika na mnayapangia muda wa utekelezaji.
Mambo zaidi ya kuzingatia katika malengo yenu;
Katika hili ni vizuri wachumba waangalie nafasi yao kifedha imekaaje, na changamoto zinazowakabili wote kwa pamoja. Je hali yao kifedha inawaruhusu kuzikabili gharama za maandalizi ya ndoa kwa ujumla. Je hali ya kimaisha ya kijana wa kiume inamruhusu wakati wowote baada ya kuchumbia aweze kufunga harusi kama anataka. Je nafasi zao kielimu zikoje, je kama zinatofautiana ni kwa kiwango gani? Na je tofauti zao kiuchumi na kitaaluma zinaweza kuwa kikwazo kwao kuoana, au kwa wazazi wao nk. Na je baada ya kuwa wamegundua na kupima uwezo wao katika hayo mambo mawili, je wanaweza wakasaidianaje ili wafike mahali pazuri wote wawili.
Vijana wengi wa kiume huwa wanakosea sana hapa, wengi huwa wanasema sitaki kuchumbia/kuoa mpaka niwe nimesha jikamilisha kiuchumi, niwe angalau na maisha mazuri. Sisi hatushauri sana dhana hii, ukweli ni muhimu kwa kijana wa kiume akjikamilisha kwa yale mambo ya msingi. Lakini fahamu kwamba kuna wakati mwingine kuendelea kwako kiuchumi, au kuvuka kwako kimaisha ni rahisi zaidi pale unapokuwa na mchumba au ndoa yako. Tunasisitiza tena ni vema wachumba wakae chini na kufikiri ni kwa namna gani wataendelezana kiuchumi na kitaaluma. Angalizo, ni vema uwe na uhakika kweli huyo mtu ni wa mapenzi ya Mungu kwa maana ya kuwa ni wa kwako kweli, maana wapo wachumba ambao wamekuwa wakisaidiana mpaka kulipiana ada, kupeana mitaji, kununuliana nyumba, magari nk, halafu mwishowe mmoja anavunja maagano, maumivu yake ni makubwa sana.
Jambo la tano – ni wakati wa matengenezo na kuzijenga nafsi zenu
Wachumba wengi huwa wanafichana mambo mengi sana wanapokuwa wachumba na matokeo yake hawayashughulikii mapema na hivyo yanakuja kuwaletea shida kwenye ndoa. Huenda kabla hujakubaliwa wewe tayari mwenzako alikuwa amesha wakubali vijana au mabinti wengine kwamba ataolewa nao au kuwaoa. Pia kama ni msichana huenda ameshawahi kubakwa, au kutokana na masumbufu ya kupata mtu sahihi na wakati mwingine kuachika mara kwa mara imefika mahali huyo msichana akasema sitaki kuja tena kuolewa. Zaidi huenda mmoja wenu huko nyuma ameshawahi kufanya uasherati au zinaa kabla hamjachumbiana. Au kuna mwingine amekuwa akisumbuliwa na tatizo la harufu, kufanya tendo la ndoa na mapepo nk.
Haya yote na mengine mengi yanayofanana na haya yana athari kubwa sana kiroho na kimwili kwenu kama wachumba na wanandoa watarajiwa kama hayatashughulikiwa vema katika kipindi hiki cha uchumba. Licha ya kuwa na athari mambo hayo yamepelekea nafsi za watu au wachumba wengi kujeruhika. Nafsi inapojeruhiwa inaharibu ndani ya mtu mfumo wa kufanya maamuzi, mfumo wa utiifu kwa Mungu wake, mfumo wa kunia na kuhisi pia. Sasa mifumo hii inapoharibika inapelekea watu kufanya maamuzi ambayo yapo nje ya mapenzi ya Mungu kabisa. Nawajua baadhi yao ambao wameacha na wokovu, na, wengine wamekata tamaa ya kuolewa, wapo walioamua kuolewa na mataifa ilimradi ameolewa nk.
Hivyo basi tumieni wakati huu kufanya matengenezo na kujengana nafsi zenu kwa maana ya kuombeana sana, pili kwa kuongeza ufahamu wenu katika neno la Kristo hasa maandiko yanayolenga uponyaji katika nafsi zenu, tatu kufuta na kufisha mapatano/maagano yote ambayo mmoja wenu aliyafanya huko nyuma na watu wengine na pia kufuta picha za kubakwa na kujenga ufahamu wa mtu aliyeathirika kisaikolojia kutokana na mambo kama hayo kwa njia ya Damu ya Yesu. Hatua hizi zitawasaidia kurejesha mifumo iliyoharibika na kuziruhusu nafsi zenu zifanye kazi kama inavyotakiwa.
Jambo la sita – ni wakati wa kujua taratibu mbalimbali kuelekea kwenye ndoa
Tumeshasema, kila dhehebu au kabila wana taratibu zao kuhusu uchumba hadi ndoa. Hivyo ni vema wachumba, wakafuata taratibu ambazo zimewekwa na makanisa yao hasa zile ambazo zipo katika mapenzi ya Mungu. Lakini pia lazima tukubali kwamba kuna baadhi ya taratibu za makanisa, makabila na hata madhehebu ambazo nyingine zipo tu lakini hazitekelezeki na nyingine hazimpendezi Mungu.
Sasa ni vema wachumba wazijue hizo taratibu na wajue je wanaweza kuzitekeleza au la, na kama hawawezi wafikirie kabisa wanafanyeje. Mfano kuna baadhi ya makanisa ambayo hayaruhusu mtu wa kwao aoe au kuolewa na mtu wa nje ya dhehebu hilo. Sasa hii ina maana kama una mchumba wa aina hiyo jipange kujibu maswali ya wazee wa kanisa na Mchungaji vizuri. Na zaidi kuna baadhi ya makabila na familia hazitaki uoe au kuolewa na watu nje ya kabila lako, au aliyekuzidi umri kama wewe ni kijana wa kiume nk. Hivyo ni vema kuzijua hizo taratibu ili mjue mnajipangaje kukabiliana nazo. Ushauri wetu ni huu kama una uhakika huyo mtu ni wa kutoka kwa Mungu basi simamia la Bwana maana lipi jema, kumpendeza Mungu au wanadamu?. Kumbuka Mungu ndiye mwenye ratiba ya kila mmoja wetu.
Suala la kukagua/kupima afya zenu kwa pamoja.
Kwa mazingira ya ulimwengu wa sasa suala la ukimwi limechukua sura mpya na kuleta mtafaruku ndani ya kanisa hasa kwa vijana wanochumbia kabla ya kupima afya zao. Siku hizi jambo hili limewafanya wachungaji kuomba sana kwa habari ya vijana ndani ya kanisa. Sasa kama mlikuwa hamjapima afya zenu mpaka mmechumbiana basi chukueni hatua mwende kupima. Ni vema wachumba wakapima mapema afya zao ili jambo hili lisije likawaletea shida baadaye, maana kwa sheria ya nchi yetu wachungaji hawaruhusiwi kufungisha ndoa kama mmoja wa wahusika ameathirika.
Upimaji wa afya zenu ni wa muhimu kwani, ndani ya makanisa kuna rekodi ya vijana wengi tu ambao wameshaathirika na huenda si kwa sababu ya zinaa, maana kwa mujibu wa watu wa afya njia za maambukizi ni nyingi. Kuna wengine wamezaliwa nao, kwa nia ya kuongezewa damu,kutumia vifaa kama nyembe, sindano nk. Hata hivyo swali la msingi inabaki kwamba je, liko tumaini kwa mtu aliyeathirika kuoa au kuolewa?
Tukueleze hivi, hakuna jambo gumu lolote la kumshinda Bwana, hii ni pamoja na ukimwi, kama Mungu alimfufua Lazaro, alitenganisha bahari ya Shamu na watu wakapita, kama Yesu alitembea juu ya maji, basi naomba ujue kwamba Ukimwi hauwezi kuzuia kusudi la Mungu hapa duniani kwa wale awapendao na kwa sababu hiyo tunasema hata kama mtu ana ukimwi na Mungu bado ana kazi naye hapa duniani, hakika atamponya huo ukimwi na atampa mke au mme.
Faida na lengo la kupima ni hili, hata kama majibu yatatoka mmoja ameathirika isiwe mwanzo wa ninyi kuachana. Kama mna uhakika Mungu aliwaanganisha huu ndio wakati wa kurudi mbele za Mungu kwa maombi ya uponyaji na kujipanga zaidi juu ya hilo.
Jambo la saba – ni wakati wa kuongeza ufahamu wenu kuhusu nafasi yako kwenye ndoa.
Je umeshawahi kujiuliza ni kwa nini Mungu anakupa mke au mme? Yamkini zipo sababu nyingi lakini baadhi yake ni; Mungu anakupa mke kama msaidizi, mlinzi, na pia unapopata mke au mme unakuwa umejipatia kibali kwa Bwana na pia ni kwa sababu ya zinaa ndio maana unahitaji mwenzi. Hizi ni baadhi ya sababu zilizoko ndani ya Biblia. Hivyo basi tafuteni wanandoa mnaowaamini na zaidi waliokoka muwaulize kuhusu wajibu wa kila mmoja kwa nafasi yake kwenye ndoa. Katika hili baadhi ya makanisa huwa yana utaratibu wake wa nani atahusika na maelekezo ya aina hii kwa wachumba. Hivyo kama kanisa lako lina utaratibu huo, fuata huo utaratibu.
Katika ndoa kuna mambo mengi sana ambayo mtatakiwa kufanya, ni vema kufuata mwongozo na ushauri wa viongozi wenu au wachungaji wenu kuhusu nini mnatakiwa kufanya katika ndoa yenu. Angalizo hapa ni hili, uwe makini na vyanzo vya ushauri au mafunzo katika eneo hili ili lisije kuleta madhara baadae. Usitafute wala kufuata kila ushauri, bali sikiliza pia uongozi wa Mungu ndani yako.
Jambo la nane– Msifanye tendo la ndoa, maana jambo hili litaharibu mpango wa Mungu na kusudi lake kupitia ninyi.
Wakati wa uchumba, si wa kufanya mapenzi au kufanya michezo ya mapenzi. Tunarudia tena ili kuonyesha msisitizo kwamba chonde chonde jamani, uchumba sio ndoa, maana uchumba unaweza kuvunjika. Hairusiwi kabisa kwa wachumba kufanya mapenzi kwa maana ya tendo la ndoa kabla ya ndoa. Kitendo cha Mungu kukujulisha/kukupa huyo mwenzako kama mke/mume mtarajiwa haina maana mna haki ya kufanya mambo ya wanandoa. Mungu kukupa huyo mwenzako sasa ni taarifa kwamba huyu ndugu ndiyo atakuwa mkeo au mmeo na anakupa taarifa sasa ili ujipange kufanya mambo ya msingi mnayotakiwa kuyafanya katika kipindi cha uchumba. Kipindi cha uchumba ndicho kipindi ambacho wachumba wengi sana wanavuruga kusudi la Mungu, na kuharibu maisha yao ya baadae na ndoa yao kwa ujumla.
Ndoa nyingi sasa hivi zina migogoro kwa sababu wakati wa uchumba walidiriki kufanya tendo la ndoa. Vijana wengi hawajajua kufanya tendo la ndoa kipindi cha uchumba lina madhara gani kwao na ndio maana wengine wanafanya. Biblia inasema katika Mithali 6:32 “Aziniye na mwanamke hana akili kabisa, afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake mwenyewe”. Hata kama ukifanya tendo la ndoa na mchumba wako ambaye mlibakiza siku moja kufunga harusi, bado umezini.
Ndani ya nafsi ya mtu kuna akili, hisia, nia na maamuzi. Biblia inaposema afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake ana maana hii, dhambi hii inapofanywa, ina haribu mfumo wa utiifu na uamnifu kwa Mungu wako, inapelekea kukosa usikivu wa rohoni kabisa, ina haribu mfumo wa kufikiri, kunia na kufanya maamuzi. Na kwa sababu hiyo si rahisi tena kusikia na kutii uongozi wa Roho Mtakatifu. Kwa watu ambao wamezoea kuwa na mahusiano mazuri na Mungu watanielewa ninachosema hapa.
Zaidi kuna baadhi ya wachumba kweli hawafanyi tendo la ndoa bali wanafanya michezo ya mapenzi. Michezo ya mapenzi (Fore play) ni maalum kwa ajili ya wanandoa, na ni sehemu ya tendo la ndoa. Hivyo kufanya michezo ya mapenzi ni kufanya mapenzi kwa sababu ile ni sehemu ya mapenzi. Kuna vitu unavichochea, unaamusha hamu ya mapenzi au unayachochea mapenzi. Biblia inasema katika Mhubiri 2:7 “Nawasihi, enyi binti za Yerusalemu, kwa paa na kwa ayala wa porini, msiyachochee mapenzi, wala kuyaamsha, hata yatakapoona vema yenyewe.”
Mungu pia anachukia michezo ya mapenzi soma Isaya 57:4-5 “Mnafanya dhihaka yenu juu ya nani, juu ya nani mmepanua vinywa vyenu, Na kutoa ndimi zenu? Je, ninyi si wana wa uasi, uzao wa uongo; ninyi mnaowasha tamaa zenu kati ya mialoni, chini ya kila mti wenye majani mabichi….. Wachumba wengi hawajui haya kwa sababu si makanisa yote yanayofundisha maswala ya mahusiano ya wachumba kimpana.
Mpaka hapa tunaamini umeshajua hasara za jambo hili na utazijizuia kabisa kulifanya. Michezo ya mapenzi ni pamoja na kunyonyana ndimi, kushikana sehemu ambazo zinaamsha ashiki ya mapenzi kama sehemu za siri, matiti, kiuno nk, pamoja na kuangalia picha za ngono. Katika kipindi ambacho tumemtumikia Mungu kupitia vijana tumejifunza na kukutana na kesi mbalimbali za aina hii na kuona namna Shetani anavyovuruga mpango wa Mungu kwa vijana. Mwenye sikio na asikie neno ambalo Roho wa Bwana awaambia vijana ili kulida kusudi la ndoa.
Ni imani yetu kwamba mambo haya nane yameongeza ufahamu na hivyo kuwa maarifa ya kutosha kukusaidia kuenenda kwa mapenzi ya Mungu katika kipindi cha uchumba.
Subscribe to:
Posts (Atom)
-
SOMO: TAMBUA MAJIRA NA NYAKATI Luka 19:41-46 41 Alipofika karibu aliuona mji, akaulilia, 42 akisema, Laiti ungalijua, hata wewe katika...
-
SHETANI ANAWEZA KUTUMIA KAZI YA MTU KUMLETEA MTU HUYO UHARIBIFU. Bwana YESU atukuzwe ndugu yangu. Karibu tujifunze Neno la MUNGU. L...
-
Katika Biblia, imeelezwa kuwa Sodoma na Gomora iliangamizwa na Mungu kwa sababu wakazi wa miji hiyo walizoelea maisha ya dhambi. Kwa mujib...