MAZINGIRA YA
DHAMBI/KUJIKUTA UMEMTENDA MUNGU DHAMBI
1.KUWA MSOMAJI WA NENO LA MUNGU
Ukimpa Mungu nafasi katika maisha yako,ukawa na muda wa kusoma Neno,kujifunza,kuhudhuria kanisani kujifunza Neno la Mungu,utakuwa na mazingira mazuri ya kushinda dhambi kwa sababu pia uwepo wa Roho Mtakatifu utakuwa nawe ukikuongoza katika hatua zako na wewe mazingira ya uovu utayachukia kabisa.NENO LA KRISTO LIKIWA KWA WINGI NDANI YAKO NA UKALIISHI,UTAKUWA MSHINDI.
2.CHAGUA RAFIKI AMBAE HAWEZI KUKUANGUSHA KIIMANI
Rafiki anaweza akawa ni chanzo au mtego wa kukupeleka kwenye uovu na kujikuta unamwacha YESU,na kuingia katika njia ya upotevu wa kumtenda Mungu dhambi.Hivyo kama ni dada uwe na marafiki walio simama kiimani na wenye hofu ya Mungu,na hata kaka pia.Kuwa na marafiki ambao wanawaza wanaume wa kuwachuna au kuuza miili yao,hawa wana weza kukupelekea imani kuacha kwan watakuwa wamekutengenezea mazingira ya wewe kuitamani dhambi na kujikuta umeingikutenda dhambi.
3.KUFUNGA NA KUOMBA
Kufunga na kuomba ni muhimu sana kwa mkristo yoyote yule,tunaona pia hata Y
esu Kristo nae alifunga (Mathayo 4:1-12.
Tunaona kuwa ingawa Yesu alikuwa kwenye njaa kali,aliweza kumshinda ibilis,hivyo kuishi maisha ya maombi,kunatupa nguvu ya ushindi katikamagumu yote.
4.MSHIRIKISHE MUNGU KATIKA KUMPATA MWENZI WAKO/NDOA YAKO
Maisha ya mahusiano ya uchumba hadi ndoa,huadwa na changamoto nyingi sana,ambazo kama Mungu hujamhusisha,unaweza kujikuta umeanguka kwenye dhambi.Kama bado hujaoa/hujaolewa hakikisha unamshirikisha sana Mungu kwenye suala zima la kumpata mme/mke sahihi kwenye maisha yako,
( Ebr 13:4)....Ndoa na iheshimiwe na watu wote,na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi Mungu atawahukumia adhabu.
Ukimpata mchumba asie na hofu na Mungu,atakuweka kwenye mazingira ya kuweza kumtenda Mungu dhambi au kufanya jambo lolote ambalo litaharibu mahusiano yako na Mungu.
Pia hata ndoa nayo/wanandoa mnatakiwa kuishi maisha kila siku ya kuwa karibu na Mungu kila siku ili msije mkaingia kwenye majaribu ya kumtenda Mungu dhambi.
ITAENDELE
No comments:
Post a Comment